Ndoto kuhusu Mbwa 

Kama ukiota kuhusu mbwa, ndoto hii inaweza kuashiria jambo jema ikiwa kama mbwa huyo ana tabia njema na anakutii, hasa mbwa mtoto. Hata hivyo, kama mbwa huyo anaonyesha tabia mbaya, anapigana ama anavunjavunja vitu, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba utaingia matatizoni hivi karibuni hasa kutokana na watu wasio waaminifu. Kama mbwa huyo akikung’ata, basi kunaweza …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Kifo 

Ndoto zinazohusu kifo zinaweza kuashiria mauti halisi ama zisiashirie kabisa roho ya mauti. Mauti inayozungumziwa kwenye ndoto si lazima iwe mauti ya kimwili. Inaweza kuwa mauti ya kiroho, mauti ya kiuchumi, mauti ya kifikra, mauti ya mahusiano n.k. Ukiota kwamba ndugu au jamaa yako amefariki, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba unapitia shambulizi fulani la kiroho.  …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu bahati mbaya 

Ndoto zinazohusu bahati mbaya kwa kawaida huwa hazihitaji mtu kuzitafsiri ama kuzifafanua sana kwani maana zake huonekana waziwazi – kile kinachotokea kwenye ndoto ndicho kile kitakachoweza kutokea maishani. Hata hivyo, kupitia ndoto za usiku, mababu zako wanaweza kukuonyesha kuwa kuna mambo mazuri ama mabaya yanayoweza kukupata, au yanayoenda kukupata. Ndoto ni muhimu, usisahau ndoto zako …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Ng’ombe 

Kama ukiota kuhusu ng’ombe ama ndama, maana ya ndoto hiyo itategemea kama unaweza kudhibiti wanyama hao au la. Kama ukiota kwamba wanyama hao wapo malishoni, ama kwamba unawachunga, ndoto hiyo inaweza kuashiria mafanikio na bahati njema siku zako zijazo. Hata hivyo, kama ukiota kwamba mifugo hiyo inakukimbiza, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba maadui zako wamekuroga …

Soma zaidi

Kuota kuhusu Watu Waliofariki 

Ukiona watu waliokwishafariki kwenye ndoto, jambo hili kwa kawaida huwa si jambo zuri kwako. Kama watu hao wamerudi kwenye ulimwengu wa walio hai, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna jambo baya lililo njiani kukujia. Kama watu hao ni ndugu zako, basi ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba unapaswa kuacha kufanya mambo maovu, la sivyo utaingia matatizoni. …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Pesa 

Kuota kuhusu pesa humaanisha kuwa na uwezo wa kutimiza madhumuni yako ama malengo yako. Malengo yako yanaweza kuhusiana na akili, hisia, ama kufika kiwango cha kuishi maisha unayoyataka. Unaweza kufikiri, kuhisi na kufanya chochote kile unachokitaka maishani. Pesa inaweza kuashiria uwezo.  Katika upande chanya, pesa huwakilisha uwezekano, mamlaka na fursa, pamoja na hali ya kujiamini …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu kuyashinda Magumu ama Kushinda Vitu

Ni muhimu unapoota ndoto fulani mara kwa mara, uweze kuelewa ndoto hiyo inamaanisha nini. Ndoto inaweza kutabiri jambo linaloweza kutokea, hivyo ni muhimu uelewe maana yake. Kwa kawaida, ndoto zinaweza kuwakilisha mawasiliano ya mababu zako na wewe. Kuota ndoto mbaya mara kwa mara si jambo zuri, kwani  linaweza kuashiria hatari. Kuna imani kwamba, ikiwa utafanya …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu nyoka

Kama ukiota kuhusu nyoka, ndoto hii inaweza kuashiria mambo mabaya siku zako za mbeleni. Inaweza kuashiria kwamba mababu zako hawajafurahishwa na wewe na kwamba kuna mtu atakusaliti, hasa ikiwa kama nyoka huyo atakung’ata kwenye ndoto hiyo. Ndoto zinazohusu nyoka hutafsiriwa katika namna mbalimbali kutegemeana na mambo mengi! Kuna watu wanaoamini kuwa nyoka katika ndoto hubeba …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu gari

Kama ukiota kwamba wewe ni abiria katika gari linaloendeshwa kwa kasi sana, mara nyingi hili hutafsiriwa kuwa ishara ya bahati njema na mafanikio. Hata hivyo, ndoto hii inaweza pia kuashiria hasara ya kifedha inayoweza kukupata siku zijazo. Ukiota kwamba unashuka kutoka kwenye gari, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba unakaidi kufanya jambo fulani ama umekataa kufuata …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Maji

Kuota kuhusu maji kunaweza kumaanisha mambo kadha wa kadha, chanya na hasi pia. Kunaweza kuashiria wasiwasi ama hofu unayoipitia, pengine kutokana na mambo yasiyotarajiwa. Maji yanaweza pia kuashiria uwepo wa hisia hasi, kama vile woga au dhamira mbaya, pamoja na mawazo na hisia hasi ambazo hazijashughulikiwa. Hali ngumu zinazoweza kuibua vikwazo, sintofahamu, mushkeli, ama mabadiliko …

Soma zaidi