Ndoto kuhusu Kifo 

Ndoto zinazohusu kifo zinaweza kuashiria mauti halisi ama zisiashirie kabisa roho ya mauti. Mauti inayozungumziwa kwenye ndoto si lazima iwe mauti ya kimwili. Inaweza kuwa mauti ya kiroho, mauti ya kiuchumi, mauti ya kifikra, mauti ya mahusiano n.k.

Ukiota kwamba ndugu au jamaa yako amefariki, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba unapitia shambulizi fulani la kiroho. 

Watu wengine huamini kwamba, kama ukiota kuna sherehe fulani nyumbani kwenu, au kuota watu wengi wamekusanyika nyumbani kwenu, ingali kuna mtu aliye mgonjwa kwenye familia yako, basi ndoto hiyo itakuwa inaashiria kwamba mtu huyo mgonjwa atafariki hivi karibuni.

Ukiota kwamba mtu fulani amefariki, baadhi ya watu huamini kwamba ndoto hiyo huja kama ishara inayoashiria kwamba kuna mtu wako wa karibu, iwe ni familia yako, ndugu yako au rafiki yako atakayepoteza maisha hivi karibuni. Mtu huyo si lazima awe ni mtu yule yule uliyemwona katika ndoto hiyo.

Ukiota unauza nyumba, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba kuna roho ya mauti imeingia maishani mwako na hivyo wewe au mtu wako wa karibu anaweza kupoteza maisha.

Wengine huamini kwamba, ukiota kwamba umekufa, ndoto hii humaanisha kwamba jambo zuri litakupata hivi karibuni. Unaweza kuolewa na mtu tajiri ama kupata mahusiano yenye mafanikio ikiwa kama bado hauna mwenza.

Leave a Reply