Ndoto kuhusu Umri

Kama ukiota kwamba una umri mdogo wakati sivyo, ndoto hii humaanisha kuwa unaweza kupatwa na ugonjwa hivi karibuni. Kama una umri mdogo na kisha ukaota kwamba umekuwa mzee, unaweza kukumbana na magumu maishani mwako siku za hivi karibuni.

Ndoto kuhusu Rangi ya Kucha

Kuota kuhusu kupaka rangi kucha zako ama kucha za mtu mwingine kunaweza kumaanisha kwamba kuna watu wanakuteta. Kama ukiota kwamba mtu mwingine anapaka kucha zako rangi, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba utamteta mtu kutokana na kumuonea wivu. Kama wewe ni mwanamke na ukiota kwamba kucha zako zinapakwa rangi, hilo linaweza kumaanisha kuwa utajuta kumzungumzia mtu …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Macho

Kama ukipoteza moja la macho yako kwenye ndoto, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba kuna hatari nyumbani mwako nawe unapaswa kuwa makini. Kama unalia kwenye ndoto, usijali, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa kuna furaha itakayokujia hivi punde. Hata hivyo, kama ukiota kuwa unahitaji kuvaa miwani, hili humaanisha kwamba mtu unayedhani kuwa unaweza kumuamini atakusaliti siku za …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Uso

Kama ukiota kuhusu uso wako, ndoto hii inaweza kumaanisha mambo kadha wa kadha. Kama uso huo ni mpana na umevimba, hili humaanisha kwamba unaweza kupata utajiri na umaarufu siku za mbeleni. Lakini kama uso huo ni mwembaba na umedumaa, basi hili humaanisha kwamba unaweza kuingia matatizoni hivi punde. Kama ukiota kuwa unaosha uso, hili humaanisha …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Vidole na Mikono

Kama ukiota kwamba mikono yako ni michafu, ndoto hii humaanisha kuwa unashawishiwa kufanya jambo baya. Kama mikono hiyo si michafu tu bali inanatanata pia, inaweza kumaanisha kwamba unaweza kuwa fukara kutokana na kile unachoshawishiwa kufanya. Kama mkono au vidole vyako vinaonekana kuumizwa kwenye ndoto, hilo linaweza kumaanisha kwamba utapoteza kazi yako siku za usoni. Kama …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Kichwa

Kama ukiota kwamba una kichwa kikubwa, unaweza kupata bahati njema siku za hivi karibuni. Kama ukiota kuwa mtu amekata kichwa chako, unaweza kupoteza mtu wa karibu yako hivi punde.

Ndoto kuhusu Moyo

Kama ukiota kuhusu moyo wako, mahusiano yako yanaweza kufikia ukomo siku za hivi karibuni nawe utaumizwa sana.

Ndoto kuhusu Sharubu

Kama ukiota kuhusu sharubu, ndoto hii huashiria kwamba utakutana na vita siku za mbeleni lakini utaweza kuishinda, ilmradi tu uwe umehakikisha kuwa unafanya jambo sahihi.

Ndoto kuhusu Mdomo

Kama ukiota kuhusu mdomo wako na kwamba kinywa chako kinatoa harufu mbaya, basi ndoto hiyo inaweza kumaanisha kuwa watu wanakukatia tamaa kutokana na mambo unayoyafanya. Kama ukiota kuhusu meno yako, unaweza kualikwa sehemu nzuri hivi punde. Lakini kama ukiota kwamba jino moja linang’olewa, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba kuna rafiki unayempoteza. Kama ukiota kuwa mdomo …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Mikono

Kama ukiota kwamba mikono yako ni dhaifu, ndoto hii humaanisha kuwa unaweza kudhoofika kiafya ndani ya siku zijazo. Kwa upande mwingine, kama ukiota kwamba mikono yako ni imara na yenye afya, unaweza kupata mafanikio makubwa ambayo haukuyatarajia.