Kama ukiota kuhusu uso wako, ndoto hii inaweza kumaanisha mambo kadha wa kadha. Kama uso huo ni mpana na umevimba, hili humaanisha kwamba unaweza kupata utajiri na umaarufu siku za mbeleni. Lakini kama uso huo ni mwembaba na umedumaa, basi hili humaanisha kwamba unaweza kuingia matatizoni hivi punde. Kama ukiota kuwa unaosha uso, hili humaanisha kuwa pengine unapaswa kutubu kwa jambo ulilolifanya. Kama ukiota kuwa uso wako unafanana na uso wa mtu mwingine, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba utahamia kwenye nyumba mpya ama utabadili kazi unayofanya siku za hivi karibuni.