Ndoto kuhusu kuku

Ukiota kuku wengi wanapiga kelele, basi ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba unapitia ushindani mkubwa kwenye eneo lako la kazi ama kwenye biashara yako. Ukiota kwamba kuku hao wanaingia nyumbani ama chumbani kwako, basi ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba ushindani huo umeingia kwenye familia ama kwenye ndoa yako, na wakati mwingine ndoto hii inaweza kuashiria uwepo …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Sanaa 

Ukiota unaandika barua ama taarifa fulani, basi ndoto hiyo huashiria kwamba kuna ujumbe unaopaswa kupata kutoka kwa mababu zako ama kutoka kwa muumba wako, nawe hauna budi kuutendea kazi ama kuufikisha ujumbe huo kwa mtu au eneo husika. Kama ukiota kwamba unachora ramani ya eneo fulani, basi ndoto hiyo humaanisha kwamba unatakiwa kufikiri kwa kina …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu bunduki  

Ukiota umebeba bunduki ya uwindaji, ndoto hiyo humaanisha kwamba unapitia majira ya kutafuta jambo fulani kwenye maisha, iwe ni pesa, mke, mahala pa kuishi, matibabu au jambo jinginelo. Ndoto hii huashiria uwepo wa ujasiri na nia thabiti ya kukifuatilia kile unachokitaka. Kuota watu waliobeba bunduki wakiwa wanakukimbiza ama kukufuatilia, humaanisha kwamba kuna vizuizi fulani vinavyozuia …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu mayai  

Kuna watu wanaoamini kwamba mayai katika ndoto huashiria uzao. Mtu akiota kwamba amekusanya mayai mengi bandani kwake, basi ndoto hiyo huonekana kuashiria kuwa mtu huyo atakuwa na uzao mkubwa. Hata hivyo, mtu anapoota kwamba mayai yamevunjika, basi ndoto hiyo hutafsiriwa kumaanisha kwamba uzao wa mtu huyo umeharibiwa ama kukamatwa na adui. Wengine huamini kwamba, mayai …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu bia  

Ukiota unapika au unatengeneza pombe/bia, ndoto hii huweza kumaanisha kwamba utatembelewa na mtu fulani atokaye eneo la mbali. Kama ukiota unakunywa bia kwenye eneo la baa, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba utatengeneza uadui hivi karibuni. 

Ndoto kuhusu sherehe ya harusi 

Sherehe za harusi katika ndoto mara nyingi hutafsiriwa na watu kumaanisha ujio wa msiba. Kama una mgonjwa nyumbani mwako, na kisha mmoja wa wanafamilia yako akaota ndoto inayohusu sherehe ya harusi, basi kuna wanaoamini kwamba ndoto hiyo huashiria kwamba mgonjwa huyo atapoteza maisha.

Ndoto kuhusu kupigana

Kupigana katika ndoto kunaweza kuashiria mashambulizi anayopitia mtu iwe katika ndoa yake, uchumi wake, afya yake ama eneo lingine maishani mwake. Ukiota unapigana na mtu au mnyama kwenye ndoto nawe ukamshinda, basi ndoto hii huashiria kwamba kuna adui aliyekuwa akikufuatilia, lakini sasa umemshinda na hivyo hataweza kukuumiza tena. Wakati mwingine kuota unapigana kunaweza kuashiria kwamba …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu viatu 

Kuota kuhusu viatu kunaweza kuashiria kwamba utapata mafanikio, kama viatu hivyo ni vipya na vinang’aa. Lakini kama viatu hivyo vimechakaa na kuchoka, basi ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba utakumbana na matatizo siku za mbeleni.

Ndoto kuhusu kuoga 

Ukiota kwamba unaoga, ndoto hii inaweza kumaanisha mambo mazuri au mambo mabaya. Kama maji unayoogea yametulia ama kama unaoga ukiwa bafuni kwako, ndoto hii humaanisha kwamba utapata bahati njema hivi karibuni ama utahamia eneo lingine na kupata furaha. Lakini kama ukiota unaoga nje ama unaoga kwenye maji yanayotiririka, ndoto hii huonekana kumaanisha kwamba utapatwa na …

Soma zaidi