Ndoto kuhusu moto
Ndoto zinazohusu moto zinaweza kutofautiana maana kutegemeana na muktadha wa ndoto husika. Kwa mfano:
Ndoto zinazohusu moto zinaweza kutofautiana maana kutegemeana na muktadha wa ndoto husika. Kwa mfano:
Maana ya kuota kuhusu mvua hutegemeana sana na ukubwa wa mvua hiyo na urefu wa kipindi cha kunyesha kwa mvua hiyo. Mvua ya kawaida inaweza kuashiria kwamba kuna jambo linalokujia – linaweza kuwa zawadi, lakini linaweza pia kuwa jambo baya kama ugonjwa. Dhoruba inaweza kuashiria matatizo ama ugonjwa siku zako za mbeleni, na kwamba unaweza …
Baadhi ya watu huhusisha nywele na utajiri. Hivyo wao huamini kwamba, ukiota una nywele nyingi, zilizonawiri, basi ndoto hiyo huashiria kuwa utapata utajiri mkubwa na ustawi katika siku zako za mbeleni. Hata hivyo, wapo wanaoamini kwamba ukiota kwamba wewe au mtu unayemfahamu ana nywele ndefu sana, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna mtu unayemfahamu ambaye …
Ndoto zihusuzo polisi au wanajeshi hutafsiriwa na baadhi ya watu kama kuashiria ulinzi kwenye maisha ya watu hao. Hata hivyo, wengine huamini kwamba polisi au wanajeshi hao katika ndoto huashiria vita vinavyofanyika dhidi yao maishani. Lakini wengine huamini kwamba ukiota kuhusu polisi au jeshi, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna jambo baya linaloenda kutokea.
Watu wengi huhusisha ndoto zinazohusu ngono na uwepo wa majini mbalimbali yaliyopo kwenye ulimwengu wa giza. Kama mwanaume ameota ndoto ya namna hii, basi ndoto hii hutafsiriwa kwamba kuna jini la jinsia la kike lililomkamata kijana huyo na kumfanya kuwa mume wake. Vivyo hivyo, kama binti akiota ndoto ya namna hii, basi ndoto hii hutafsiriwa …
Wengi huamini kwamba, ukiota kuwa kuna mtu anafanya uchawi dhidi yako au dhidi ya mtu mwingine, basi ndoto hii huashiria kwamba unajaribu kuonyeshwa kwamba kuna vitendo vya uchawi vinavyokuzunguka wewe ama vinavyozunguka familia yako. Mtu yule unayemwona kwenye ndoto akifanya uchawi, mara nyingi huwa si ndiye aliye mchawi kiuhalisia. Ni imani ya wengi kwamba, kwenye …
Wengi huamini kwamba, ukiota unakula nyama mbichi basi ndoto hiyo humaanisha kwamba umelishwa nyama za watu na wachawi.
Ukiota kwamba unakula nyama ya nguruwe, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba utapoteza kitu cha muhimu kwako siku za mbeleni.
Ukiota kwamba unakula maini, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba utakuwa na afya njema na thabiti.
Ukiota unakula nyama ya mwana-kondoo, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba utapatwa na bahati mbaya.