Ndoto kuhusu Homa
Kama ukiota kwamba una homa au mafua, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kuwa kuna watu wanaosubiri kujinufaisha kutokana na udhaifu wako.
Kama ukiota kwamba una homa au mafua, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kuwa kuna watu wanaosubiri kujinufaisha kutokana na udhaifu wako.
Kama ukiota kwamba mifupa yako imevunjika, kwa kawaida ndoto hii huashiria kwamba utapatwa na ugonjwa ndani ya siku zijazo. Hata hivyo, kama ni mifupa ya miguu yako ndio imehusika kwenye ndoto hiyo, hilo humaanisha kuwa utaoa/utaolewa na mtu dhaifu. Kama wewe ni mwanamke, ndoto hii humaanisha kuwa mume wako atakuwa mlevi na mvivu, asiyeweza kukusaidia …
Kama ukiota kwamba hauwezi kupumua, kwa kawaida ndoto hii huwa ishara mbaya. Humaanisha kuwa utaugua hivi karibuni.
Kama ukiota kwamba una majipu, unaweza kupatwa na ugonjwa siku za usoni. Kama ukiota kwamba mtu mwingine ana majipu, unaweza kuumizwa moyo na mtu katika siku zijazo, hasa kama mtu huyo uliyemuona kwenye ndoto ni mwenzi wako.
Kama ukiota kwamba unaweza kumsikia mtu anayezungumza na wewe lakini masikio yako yameziba, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa mababu zako wanakuita.
Kama ukiota kuhusu mtu mwenye ngozi nyeupe au zeruzeru (tunaomba radhi kama neno hili litawatatiza baadhi ya watu), ndoto hii inaweza kumaanisha bahati kwani hali hii ni hali itokeayo kwa nadra na hivyo watu wanaohusishwa nayo huwa wa kipekee. Watoto Zeruzeru Kama ukiota kwamba unamuona mtoto zeruzeru hii ni ishara nzuri inayoweza kuashiria heshima, utulivu, …
Kama ukiota kwamba umepatwa na ajali na umejeruhiwa, ndoto hii humaanisha kwamba unahitaji kuwa makini kwani jambo baya linaweza kukupata hivi karibuni. Kama ajali uliyoota inahusisha maji, unaweza kupatwa na matatizo ya kimahusiano, na kama inahusisha mtu mwingine kukuumiza, basi unaweza kuingia matatizoni kazini.
Kama ukiota kwamba wewe ni mwembamba ama umepungua sana uzito, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa kuna hofu zinazokujia. Inaweza pia kumaanisha kuwa utapoteza pesa siku za mbeleni. Hivyo, kuwa makini na namna unavyotumia pesa zako pamoja na nani unayemkopesha hela yako. Kwa upande mwingine kama ukiota kwamba wewe ni mnene sana, ndoto hiyo inaweza kumaanisha …
Kama ukiota kwamba unatokwa na damu kwa muda mrefu na haujui kwanini, ndoto hii humaanisha kuwa unaweza kupatwa na ugonjwa mbaya sana hivi karibuni. Kama unakohoa damu, unaweza kuingia kwenye ugomvi siku za hivi karibuni. Lakini kama umeota kuwa unatapika damu, hili humaanisha kuwa unaweza kuwa mtu mwenye bahati sana.
Kuota kuhusu meno kunaweza kumaanisha mambo mengi mbalimbali. Kung’oa Meno Kuota kuhusu kung’oa jino lolote kunaweza kumaanisha kwamba unaweza ukapoteza kitu muhimu kwako, kitu hicho kinaweza kuwa kazi yako ama mtu muhimu maishani mwako kama vile mtu wa familia yako. Ndoto hiyo inaweza kuhusisha meno mawili ya mbele ama unaweza kuota kwamba umeng’oa meno yako …