Kama ukiota kwamba mifupa yako imevunjika, kwa kawaida ndoto hii huashiria kwamba utapatwa na ugonjwa ndani ya siku zijazo. Hata hivyo, kama ni mifupa ya miguu yako ndio imehusika kwenye ndoto hiyo, hilo humaanisha kuwa utaoa/utaolewa na mtu dhaifu. Kama wewe ni mwanamke, ndoto hii humaanisha kuwa mume wako atakuwa mlevi na mvivu, asiyeweza kukusaidia kwa lolote. Kama wewe ni mwanaume, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa mke wako atakuwa mwanamke mwema, lakini hatakuwa imara vya kutosha kuitunza nyumba yake.