Ndoto kuhusu Kulala

Kama ukiota kwamba umelala, ndoto hii huashiria jambo baya sana. Hata hivyo, kama ukiota kuwa umeamka, hilo humaanisha kuwa kuna mtu atakutamkia kuwa anakupenda na huzuni zako zote zitaisha.

Ndoto kuhusu mikato/michano/chale za Ngozi

Kama hauumwi na kisha ukaota kwamba ngozi yako inachanwa na kisha inapakwa dawa kama inavyofanywa kwenye tiba za kienyeji, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba una adui anayejaribu kukuroga kwa kutumia dawa za kienyeji. Wakati mwingine ndoto hii inaweza kuwa inakuonya kuwa unahitaji kuamka na kutafuta msaada kwani kuna mtu anayejaribu kukuroga. Kama teyari umaumwa nawe …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Kunyoa

Kama ukiota kuhusu kunyoa ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba unahitaji kuwa makini na marafiki wanaokuzunguka kwani huenda wanajaribu kukulaghai, hasa kuhusiana na mtu umpendaye. Kama ukiota kwamba unanyoa sehemu fulani ya mwili wako, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba utaweza kupatwa na shida au maradhi kwenye sehemu hiyo. Ngozi Kama ukiota kuhusu ngozi yako, ndoto hii …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Shahawa

Kwa kawaida kuota kuhusu shahawa ni ishara mbaya inayoweza kumaanisha kuwa umerogwa ili watu wasikupende. Kuota kuhusu shahawa kunaweza kuashiria maamuzi unayopaswa kufanya, ama kunaweza kumaanisha ujasiri wa kufanya maamuzi magumu. Kuota kuwa shahawa zipo usoni mwako ama kuona shahawa juu ya uso wa mtu mwingine kunaweza kumaanisha hali ya kuaibishwa kutokana na matokeo ya …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Chunusi

Kuota kuhusu kuwa na chunusi nyingi kwa kawaida huchukuliwa kama ishara nzuri. Kunaweza kumaanisha kuwa utastawi na kuwa mtu wa kupendeza siku zijazo. Kama wewe ni kijana unayechumbia na ukaota kuhusu chunusi, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba mahusiano yako na mtu huyo unayemchumbia yatadumu. Kama wewe ni bibi harusi na ukaota kuwa unapaka mafuta kwenye …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Pua

Kama ukiota kuhusu pua yako, ndoto hiyo inaweza kumaanisha mambo mengi. Kama ukiota kwamba pua yako haipo, hii inaweza kuwa ishara ya jambo baya au hata kifo hasa hasa kama ukipata ndoto hii ilhali ukiwa unaumwa. Kama ukiota kwamba pua ni kubwa mno, unaweza kupata utajiri lakini ukahangaika kupata mpenzi, na kujikuta ukigombana na wengine …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Kujifungua Mtoto

Kama wewe ni mjamzito au umeolewa na kisha ukaota kwamba unajifungua mtoto, hili humaanisha kuwa utajifungua salama. Lakini kama wewe si mjamzito, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba kuna jambo baya linalokujia. Kama wewe ni mwanaume nawe ukiota kwamba mwenzi wako anajifungua, hili humaanisha kuwa pengine ni mjauzito.

Ndoto kuhusu Kidonda

Kama ukiota kwamba una kidonda kilichotokana na kujikata au kujijeruhi vinginevyo, hili humaanisha kwamba utapata bahati kwenye mahusiano yako (kama una umri mdogo) au kwenye biashara yako (kama una umri wa makamo). Hata hivyo, kama kidonda hicho ni kidogo tu, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba utapata bahati mbaya siku za hivi karibuni.

Ndoto kuhusu Kutapika

Kuota kuhusu matapishi kunaweza kumaanisha uchawi ama ongezeko la tabia mbaya. Wewe Kutapika Kama ukiota kwamba unatapika, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba uliwapokonya watu urithi wao. Wakati mwingine, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba unapaswa kuchukua tu kile unachohitaji maishani. Kuota kuhusu kutapika kunaweza kumaanisha kwamba unahitaji kubadili mwenendo wako kwani usipofanya hivyo utapoteza vitu vizuri …

Soma zaidi