Kama ukiota kuhusu pua yako, ndoto hiyo inaweza kumaanisha mambo mengi. Kama ukiota kwamba pua yako haipo, hii inaweza kuwa ishara ya jambo baya au hata kifo hasa hasa kama ukipata ndoto hii ilhali ukiwa unaumwa. Kama ukiota kwamba pua ni kubwa mno, unaweza kupata utajiri lakini ukahangaika kupata mpenzi, na kujikuta ukigombana na wengine mara kwa mara. Kama pua hiyo ina mwonekano mzuri, basi hiyo huwa ishara ya bahati njema na humaanisha kuwa unaweza kupata umaarufu kazini. Kama ukiona tu pua yako na hauelewi kwanini, hilo linaweza kumaanisha kwamba jitihada zako hazitazaa matunda. Aidha, kama pua hiyo inavuja damu kwenye ndoto, unaweza kuugua siku za hivi karibuni.