Ndoto kuhusu Kunyoa

Kama ukiota kuhusu kunyoa ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba unahitaji kuwa makini na marafiki wanaokuzunguka kwani huenda wanajaribu kukulaghai, hasa kuhusiana na mtu umpendaye. Kama ukiota kwamba unanyoa sehemu fulani ya mwili wako, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba utaweza kupatwa na shida au maradhi kwenye sehemu hiyo.

Ngozi

Kama ukiota kuhusu ngozi yako, ndoto hii inaweza kumaanisha mambo mazuri au mabaya kutegemeana na kile kilichotokea kwenye ngozi husika. Kama ukiota kuhusu chunusi kwenye ngozi yako, ndoto hiyo inaweza kuashiria mambo mazuri kwenye mahusiano yako. Unaweza kupata mtu hivi karibuni ama kuendelea kuwa na mpenzi wako wa sasa. Hata hivyo, kama ukiota kwamba ngozi yako inakatwa, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba mtu unayemuamini atageuka kuwa adui.

Leave a Reply