Ndoto kuhusu mikato/michano/chale za Ngozi

Kama hauumwi na kisha ukaota kwamba ngozi yako inachanwa na kisha inapakwa dawa kama inavyofanywa kwenye tiba za kienyeji, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba una adui anayejaribu kukuroga kwa kutumia dawa za kienyeji. Wakati mwingine ndoto hii inaweza kuwa inakuonya kuwa unahitaji kuamka na kutafuta msaada kwani kuna mtu anayejaribu kukuroga.

Kama teyari umaumwa nawe ukaota kwamba ngozi yako inachanwa na kisha inapakwa dawa kama inavyofanywa kwenye tiba za kienyeji, ndoto hii inaweza kuwa ishara njema kwamba utapata nafuu na utapokea msaada unaouhitaji ili kupona. Kama kwenye ndoto hiyo unamuona mganga akichana na kupaka dawa kwenye ngozi hiyo, hili humaanisha kuwa mto huyo ndiye atakayeweza kukupatia msaada utakaokuponya.

Kama chale zimechanjwa kwenye ngozi lakini hakuna dawa yoyote ile iliyopakwa, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa utakumbana na matatizo yatakayokusababishia hofu na lawama kutoka kwa watu muhimu maishani mwako.

Leave a Reply