Ndoto kuhusu Tetekuwanga
Kama ukiota kwamba una tetekuwanga, hili humaanisha kwamba utatajirika hivi karibuni.
Kama ukiota kwamba una tetekuwanga, hili humaanisha kwamba utatajirika hivi karibuni.
Kama ukiota kwamba unahisi maumivu makali, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa kuna mambo mazuri utayoyapata siku zijazo, hasa hasa katika muktadha wa fedha.
Kuota kuhusu ute/kamasi kunaweza kumaanisha jambo jema kwa baadhi ya watu, na jambo baya kwa watu wengine. Aina tofauti-tofauti za Ute Kama ukiota ute wa kijani, unaotiririka na kutia kinyaa, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa umerushiwa jambo baya kama vile ugonjwa au uchawi. Kama ukiota kwamba ute umepakwa mwilini mwako ama kwenye blangeti lako, ndoto …
Kama ukiota kuhusu kuona ama kunusa mkojo au vinyesi, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna mtu amekuroga. Kadri harufu ya kinyesi hicho ilivyo mbaya zaidi, ndivyo kadri uchawi huo unavyofanya kazi. Unahitaji kumuona mganga wa kienyeji ili kupata msaada. Kuota kuhusu Kinyesi Kuota kuhusu Mkojo
Kama ukiota kwamba mwanamke ameharibikiwa mimba, hili humaanisha kuwa mwenzi wako anaweza kukumbana na matatizo maishani mwake.
Kama ukiota kuhusu dawa, hii ni ishara ya bahati sana. Kama ukiota kuhusu dawa ya mitishamba, ndoto hii humaanisha kuwa mtu unayemfahamu, anayeugua, atapata kupona hivi karibuni. Ndoto hii inaweza pia kumaanisha kuwa utapata mafanikio siku zijazo. Kuota kuhusu vidonge vya dawa ni jambo jema pia, na humaanisha kwamba utakuwa salama pindi utaposafiri.
Kama ukiota kwamba unaugua surua, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa mbele yako kuna umaskini. Unaweza ukapoteza pesa kutokana na kumkopa mtu ambaye atashindwa kulipa, ama unaweza kuingia matatizoni kazini.
Kama ukiota kwamba una wazimu/ukichaa, hili humaanisha kuwa una bahati na utakuwa na maisha marefu yenye mafanikio. Kama ukiota kuwa mtu fulani amepata wazimu/ amekuwa kichaa, hili humaanisha kuwa hivi karibuni unaweza kupata habari zitakazokushangaza.
Kama ukiota kwamba unaugua maumivu ya sikio, hili humaanisha kwamba mababu zako wanajaribu kukueleza kitu lakini wewe huwasikilizi.
Kama ukiota kwamba unaumwa, kwa kawaida hili humaanisha kuwa utakuwa na afya. Kama ukiota kuwa una ugonjwa fulani mahsusi, hili humaanisha kuwa mtu mwingine anayeumwa ugonjwa huo atapona.