Kuota kuhusu ute/kamasi kunaweza kumaanisha jambo jema kwa baadhi ya watu, na jambo baya kwa watu wengine.
- Kama unaumwa, nawe ukaota kwamba unatokwa na makamasi, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa utapata tiba ama utapona upesi.
- Kama ukiota kwamba unapenga makamasi, hili humaanisha kuwa utajihisi vizuri zaidi pindi utakapofanya uamuzi wa kuyakabili matatizo yanayokusababishia maumivu.
- Kama ukiota kuhusu pua inayotoka makamasi mengi sana na kisha ukajihisi kuwa msafi, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa muda wako wa uponyaji utakujia hivi punde.
- Kama ukiota kuwa mtu wako wa karibu anatokwa na makamasi, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa mtu huyo anakabiliana na hali ya mfadhaiko kutokana na matatizo yasiyoisha na kwamba mtu huyo anahitaji msaada wako.
- Ni jambo baya kuota kwamba mtu aliyekwishafariki anatokwa na makamasi, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa kuna hali iliyosabbaishwa na uchawi inayopaswa kurekebishwa.
Aina tofauti-tofauti za Ute
Kama ukiota ute wa kijani, unaotiririka na kutia kinyaa, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa umerushiwa jambo baya kama vile ugonjwa au uchawi. Kama ukiota kwamba ute umepakwa mwilini mwako ama kwenye blangeti lako, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa kuna roho chafu unazorushiwa. Kama ukiota kuhusu ute mweupe, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa kazi/vitendo vyako vitakuzalishia amani, furaha na mafanikio. Kama ute huo ni mweupe sana, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa mtu mbaya anajitenga na wewe na hivyo maisha yako yatakuwa mazuri zaidi.
Kama ukiota kuhusu kupiga chafya, ndoto hii inaweza kuashiria udhaifu, ugonjwa, matatizo au hali mbaya utakazokumbana nazo, ambazo utabidi kuzitatua haraka.