Ndoto kuhusu Mkojo na Vinyesi

Kama ukiota kuhusu kuona ama kunusa mkojo au vinyesi, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna mtu amekuroga. Kadri harufu ya kinyesi hicho ilivyo mbaya zaidi, ndivyo kadri uchawi huo unavyofanya kazi. Unahitaji kumuona mganga wa kienyeji ili kupata msaada.

Kuota kuhusu Kinyesi

  • Kujiona ukiwa unatoa kinyesi kwenye ndoto kunaweza kumaanisha kwamba kuna ugonjwa ambao mababu zako wanauondoa kutoka kwako, ambao ulidhani kuwa utahatarisha maisha yako, ama kwamba kuna mambo magumu ambayo umekuwa ukikumbana nayo ambayo yataondolewa kwako.
  • Ukiota kwamba umejichafua kwa kinyesi kunaweza kumaanisha kuwa kuna mtu anayetumia uchawi kuleta migogoro kati yako na mwenzi wako.
  • Kama ukiona kinyesi kwenye ndoto – iwe kinyesi cha mtu au mbwa – ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna mtu anakuroga.
  • Kama ukiota kwamba upo chooni, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kuwa kuna watu wanapinga juhudi zako na kujaribu kuzikwamisha. Wakati mwingine, kuota kuhusu choo kunaweza kumaanisha kwamba kuna watu waovu unaopaswa kujitenga nao ili kuweza kukua kiroho.
  • Kuota kuhusu kinyesi kunaweza kumaanisha kwamba kuna mtu wa karibu yako aliye na ujauzito ama aliyepoteza ujauzito na anahitaji kutakaswa na kufanyiwa ibada ya kimila kwa ajili ya mtoto huyo aliyefariki.

Kuota kuhusu Mkojo

  • Kuota kuhusu kukojoa kunaweza kuwa kunakutahadharisha kwamba umebanwa na mkojo na hivyo unahitaji kuamka na kwenda kukojoa. Kwa kawaida hali hii huwapata watoto wanaokua ambao huenda bado wanajikojolea kitandani.
  • Wakati mwingine, kuota kuhusu kukojoa kunaweza kumaanisha kuwa kuna mtu ni mjamzito au amempatia mtu ujauzito. Inaweza kumuashiria mtu wako wa karibu auhata wewe mwenyewe.
  • Kujiota kwamba umejikojolea na nguo zako zimelowana kunaweza kumaanisha kuwa kuna mtu anakuroga akiwa na lengo la kuharibu mahusiano yako ya kimapenzi.

Leave a Reply