Kama ukiota kwamba wewe ni mwembamba ama umepungua sana uzito, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa kuna hofu zinazokujia. Inaweza pia kumaanisha kuwa utapoteza pesa siku za mbeleni. Hivyo, kuwa makini na namna unavyotumia pesa zako pamoja na nani unayemkopesha hela yako. Kwa upande mwingine kama ukiota kwamba wewe ni mnene sana, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kuwa utaugua ama utagombana na mwenzi wako.
Kuwa Mnene/ Mzito Sana
Kama ukiota kwamba wewe ni mzito/mnene sana, ndoto hiyo inaweza kuashiria jambo baya. Inaweza kumaanisha kwamba utapitia wakati mgumu wa huzuni na magonjwa. Kuota kuhusu kuwa mnene kunaweza pia kuashiria mafanikio siku za mbeleni.
Kama ukiota kwamba haufurahishwi kuhusiana na kuwa mnene, hilo linaweza kuashiria fedheha au aibu inayokujia. Kama ukiota kuhusu kuwa mzito kupitiliza kwenye eneo la kijamii, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kuwa utaaibishwa kutokana na makosa yako. Kuota kuhusu kufurahishwa na suala la kuongezeka uzito kunaweza kumaanisha kuwa utapata mali, utajiri, ustawi, na kuishi maisha bora yanayokutosheleza. Inaweza pia kumaanisha hali ya kupata heshima katika taaluma/tasnia uliyopo. Mwanamke kuota kuhusu kuwa na uzito uliopitiliza kunaweza kumaanisha kwamba mwanamke huyo ni mjamzito.