Ndoto kuhusu Kucha

Kama ukiota kuhusu kucha zako, maana ya ndoto hiyo hutegemea kama kucha hizo ni ndefu au fupi. Kama ukiota kuhusu kucha ndefu, ndoto hiyo huashiria bahati njema na huweza kumaanisha kwamba utapata utajiri siku zijazo. Ni jambo jema zaidi kuota kwamba mume au mke wako ana kucha ndefu, kwani hilo huweza kumaanisha kuwa mume au mke huyo atakuwa mchapakazi na atakutunza.

Hata hivyo, kama ukiota kuhusu kucha fupi, ndoto hii humaanisha kuwa utapoteza kitu siku za usoni. Kwa upande mwengine, kama kucha hizo ni fupi kutokana na kuzikata kwenye ndoto, hilo linaweza kumaanisha kwamba hivi punde unaweza kugombana na mtu kwenye familia yako.

Leave a Reply