Ndoto kuhusu Ng’ombe 

Kama ukiota kuhusu ng’ombe ama ndama, maana ya ndoto hiyo itategemea kama unaweza kudhibiti wanyama hao au la. Kama ukiota kwamba wanyama hao wapo malishoni, ama kwamba unawachunga, ndoto hiyo inaweza kuashiria mafanikio na bahati njema siku zako zijazo. Hata hivyo, kama ukiota kwamba mifugo hiyo inakukimbiza, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba maadui zako wamekuroga na watakushinda. Daima ndoto zinazohusu ng’ombe weusi hutafsiriwa kama ndoto mbaya, na zinaweza kuashiria matatizo kazini kwako ama kwenye mahusiano yako.

Ukiota ng’ombe wanapigana, ndoto hii huashiria kwamba kuna mtu wako wa karibu, kwenye familia, ukoo, au rafiki, atakayepoteza maisha.

Wengine huamini kwamba ng’ombe hutumiwa kama jini katika ndoto. Hivyo, ukiota unaona ng’ombe anakufuatilia ama anakukimbiza kwenye ndoto, ndoto hii humaanisha kwamba kuna roho mbaya zinazokufuatilia.

Kuna watu wanaoamini kuwa kiujumla ng’ombe huashiria nguvu za giza ama nguvu za kichawi katika ndoto.

Leave a Reply