Kama ukiota kwamba wewe ni abiria katika gari linaloendeshwa kwa kasi sana, mara nyingi hili hutafsiriwa kuwa ishara ya bahati njema na mafanikio. Hata hivyo, ndoto hii inaweza pia kuashiria hasara ya kifedha inayoweza kukupata siku zijazo.
Ukiota kwamba unashuka kutoka kwenye gari, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba unakaidi kufanya jambo fulani ama umekataa kufuata ushauri fulani.
Ukiota kwamba umenunua gari, ndoto hiyo humaanisha kwamba utapata cheo au nyadhifa fulani siku za hivi karibuni. Vivyo hivyo, ukiota umeuza gari ama umepoteza gari, basi ndoto hiyo humaanisha kwamba hivi karibuni utapoteza cheo ama kupata hasara fulani maishani mwako.
Ukiota kwamba una safari fulani, umetayarisha na kufungasha vitu vyako vyote kwa ajili ya safari hiyo. Kisha unapopanda tu gari hilo kwa ajili ya kuanza safari, ghafla unakumbuka kwamba kuna kitu fulani umesahau nyumbani na hivyo ukageuza na kurudi nyumbani kwako na unaporudi kituoni ukakuta gari au basi limekwishakuacha, basi ndoto hii hutafsiriwa kumaanisha kwamba siku yako ya kuondoka hapa duniani bado haijawadia na kwamba bado una siku nyingi za kuishi hapa duniani. Lakini kama ukifanikiwa kupanda gari hilo na kuanza safari basi ndoto hiyo huonekana kumaanisha kwamba siku zako au za mtu wako wa karibu, za kuishi hapa duniani, zinafikia ukingoni.