Ndoto kuhusu ngono

Ndoto kuhusu ngono mara nyingi huwa si ndoto nzuri kwani huashiria roho chafu zinazokuzunguka, zinazozunguka maisha yako ama zinazozunguka mahali unapolala. Hali hii inaweza kusababishwa pindi uchawi unapotumika dhidi yako ama pale unaporushiwa roho chafu. Hivyo basi, ili kupigana na ndoto hii na kutatua tatizo hili, hasa pale ndoto hii inapojirudia mara kwa mara, itakubidi …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu kurogwa / uchawi

Kama mtu, kama vile mchawi, akikuroga, inaweza kuwa kwamba anakuonea wivu wewe na kukionea wivu kile ulichonacho maishani mwako, na kwamba anataka jambo baya likupate, kama vile ajali au kifo. Wengi huamini kwamba, ukiota kuwa kuna mtu anafanya uchawi dhidi yako au dhidi ya mtu mwingine, basi ndoto hii huashiria kwamba unajaribu kuonyeshwa kwamba kuna …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu nyama mbichi 

Kama ukiota kwamba kuna mtu amekupatia nyama mbichi, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba mpinzani wako wa kimapenzi anakuroga. Kama umeoa/umeolewa hivi karibuni, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba haujapokelewa na mababu wa familia yako mpya.  Wengine huamini kwamba, ukiota unakula nyama mbichi basi ndoto hiyo huashiria kwamba wachawi wamekulisha nyama za watu.

Kuota kuhusu kula nyama ya ng’ombe

Kama ukiota kwamba unakula mnofu, mchuzi au supu ya nyama ya ng’ombe, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba jambo baya au hasara iko njiani kukupata. Ukiota unakula nyama, ndoto hii huashiria vitendo vya nguvu za giza. Mara nyingi, kula nyama kwenye ndoto huhusishwa na kula nyama za watu katika ulimwengu wa giza. Pia, ndoto hii huashiria …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu chakula  

Kuota kuhusu chakula kunaweza kuwa na maana nyingi kutegemeana na kile unachokifanya na chakula hiko.  Kununua chakula  Ukiota kwamba unanunua chakula, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa utapokea kitu fulani hivi karibuni, hasa kama chakula hiko kimepikwa ama ni chakula cha kubebeka (takeaway).  Kula chakula  Watu wengi wanaamini kwamba, kula chakula ama kulishwa chakula katika ndoto …

Soma zaidi