Kuota kuhusu chakula kunaweza kuwa na maana nyingi kutegemeana na kile unachokifanya na chakula hiko.
Kununua chakula
Ukiota kwamba unanunua chakula, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa utapokea kitu fulani hivi karibuni, hasa kama chakula hiko kimepikwa ama ni chakula cha kubebeka (takeaway).
Kula chakula
Watu wengi wanaamini kwamba, kula chakula ama kulishwa chakula katika ndoto si jambo zuri. Wengi huhusisha ndoto hizi na mambo ya kishirikina. Mtu anapoota kwamba amekula chakula fulani kwenye ndoto, wengi huamini kuwa mtu huyo amelishwa vyakula vichafu na wachawi ama maadui wa kiroho.
Kula Kupitiliza / Kuvimbiwa
Ukiota kwamba umekula chakula kingi sana hadi ukajihisi kuvimbiwa, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba umekuwa maskini.