Ndoto kuhusu ngono

Ndoto kuhusu ngono mara nyingi huwa si ndoto nzuri kwani huashiria roho chafu zinazokuzunguka, zinazozunguka maisha yako ama zinazozunguka mahali unapolala. Hali hii inaweza kusababishwa pindi uchawi unapotumika dhidi yako ama pale unaporushiwa roho chafu. Hivyo basi, ili kupigana na ndoto hii na kutatua tatizo hili, hasa pale ndoto hii inapojirudia mara kwa mara, itakubidi kutumia mfumo wako wa imani. Unaweza kutafuta msaada kwa kuwaona waganga wa kienyeji ama kujikita katika maombi kama wewe ni mtu unayemuamini Mungu. 

Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia kwamba, kama wewe ni mvulana ama msichana unayeingia utu uzima/unayebalehe, ndoto hii inaweza kuwa ishara tu ya kupevuka kwako na kufikia umri wa kubalehe, kwani katika umri huo wewe hufikia kilele cha kwanza cha msisimko wa kingono kabla ya kuamka, na hivi ndivyo unapogundua kwamba una uwezo wa kupata watoto na kuwa mzazi siku za mbeleni. 

Watu wengi huhusisha ndoto zinazohusu ngono na uwepo wa majini mbalimbali yaliyopo kwenye ulimwengu wa giza. Kama mwanaume ameota ndoto ya namna hii, basi ndoto hii hutafsiriwa kwamba kuna jini la jinsia la kike lililomkamata kijana huyo na kumfanya kuwa mume wake. Vivyo hivyo, kama binti akiota ndoto ya namna hii, basi ndoto hii hutafsiriwa kwamba kuna jini la jinsia ya kiume lililomkamata binti huyo na kumfanya kuwa mke wake. Watu wengi hulifahamu jini hili kama jini mahaba.

Watu huamini kuwa kama mtu asiye na mume/mke akiota ndoto za namna hii, hasa hasa ikiwa kama ndoto hizi zitajirudia mara kwa mara, basi mtu huyo anaweza asioe/asiolewe kamwe kwani atakuwa amekwishaoa/kuolewa kwenye ulimwengu wa giza, na hivyo majini hayo hayatamruhusu mtu huyo kuoa mtu mwingine ama kuolewa na mtu mwingine.

Leave a Reply