Ndoto kuhusu ujauzito / mimba

Ndoto zinazoashiria mimba/ujauzito:

  • Kama ukiota kuhusu matunda mengi mbalimbali, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa ndugu au rafiki yako ni mjamzito. 
  • Kama ukiota kwamba unakula tunda fulani, basi wewe ndio unaweza kupata ujauzito ama pengine teyari u mjamzito. 
  • Kama ukiota kwamba unaogelea kwenye maji machafu ama yenye matope, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba wewe ni mjamzito.
  • Kama ukiota kwamba una ujauzito, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba siku moja utazaa watoto mapacha, hasa ikiwa kama ndoto hiyo itajirudia tena. 
  • Ukiota kwamba unamuona mtoto amebeba mtoto, basi ndoto hii humaanisha kwamba kuna baraka ya mtoto inayokujia ama inayomjia mtu wa karibu yako.
  • Ukiota kwamba wewe ni mjamzito, basi ndoto hii humaanisha kwamba kuna ndugu au jamaa yako ambaye ni mjamzito ama atapata ujauzito.
  • Ukiota una ujauzito na tumbo lako limekuwa kubwa sana, ndoto hii huashiria kuwa kuna jambo maishani mwako linalozaliwa upya. Jambo hili linaweza kuwa huduma yako, kazi yako, mahusiano yako n.k.
  • Kama ukiota kuhusu miwa mingi, mirefu, iliyonawiri na kustawi, basi ndoto hii huashiria kwamba wewe au mtu wako wa karibu ni mjamzito.

Baadhi ya watu wanaweza kuota ndoto kuhusu ujauzito wao wenyewe, hata hivyo mara nyingi ni mtu mwengine ndiye huota ndoto kuhusiana na ujauzito wako.

Majukumu na Baraka za Mababu

 Zipo ndoto ambazo, ingawa unajijua na watu wengine wanafahamu kwamba u mjamzito, mtu wa makamo kwenye familia yako anaweza kuoteshwa kuhusiana na jinsia ya mtoto huyo. Ipo imani kwamba, ikiwa ndoto ya namna hiyo itatokea, basi hilo litamaanisha kwamba mtoto huyo ajaye ni baraka kutoka kwa mababu zako. Hata hivyo, tatizo hutokea pale mtoto anapozaliwa na kuonyesha dalili za ugonjwa. Hasa hasa, ikiwa kama ‘sadaka’ hazikutolewa na familia ya baba husika. Mtoto anaweza kuwa mlemavu. Na wewe, kama mzazi, utapaswa kumshukuru mtoto huyo pindi anapozaliwa kwani mtoto huyo hubeba bahati njema. Kabla mtoto hajatolewa nje ili kutizamwa na majirani na jamaa, mambo kadhaa sharti yafanyike kwanza, kama vile kuandaa pombe ya kimila na kupika viungo vya ndani vya mnyama fulani.

Kuna ndoto ambazo tunafahamu fika kwamba, zinapokujia kuna mambo utapaswa kuyafanya ili kuepusha mambo mabaya kutokea. Hata hivyo, ndoto zihusuzo kifo na ujauzito zinapokujia, hakuna lolote unaloweza kulifanya ili kuepusha kile kilichotokea. Lakini ni muhimu kuikumbuka ndoto uliyoiota usiku, kwani kuikumbuka ndoto hiyo kunaweza kukusaidia. 

Kuota kuhusu Ujauzito wa Mtu Mwengine

Kuota kuhusu mtu mwingine kuwa mjamzito ni ishara kwamba kuna mambo au vitu vilivyo haki yako lakini vimeshikiliwa na mikono ya mtu mwingine. Hata hivyo, hivi punde tu vitu hivyo vitarudi mikononi mwa mtu sahihi. Vitu hivyo vinaweza kuwa vitu ulivyovirithi ama vitu ulivyovipoteza siku za nyuma. Ndoto hii inaweza pia kumaanisha kuwa nafasi fulani ya ajira iliyopatiwa kwa mtu mwingine pasivyo haki i njiani kufichuliwa, na kurejeshwa kwako.

Kuna watu wanaamini kuwa, unapoota kuhusu mtu fulani kuwa mjamzito basi ndoto hiyo humaanisha kwamba, kuna mtu unayemfahamu amepata ujauzito ama atapata ujauzito, ama vinginevyo, wewe ndiye utakayepata ujauzito hivi karibuni. Hata hivyo, mtu yule uliyemuona kwenye ndoto si lazima awe mtu yule atakayepata ujauzito kwenye maisha halisia.

Leave a Reply