Ndoto kuhusu Udongo

Kuota kwamba uko shambani ama kwenye bustani ndogo ukichimba udongo, ukiotesha ama ukilima, kunaweza kuashiria kwamba kuna mtu aishiye nyumbani kwako atakayepatwa na maradhi, ama kuugua homa au kifua. Kuota kuhusu uwepo wa kifusi cha udongo wa kujengea nyumbani kwako ni ishara mbaya inayoweza kuashiria ugonjwa.

Kuota kwamba unachimba shimo ama kaburi na kugeuza-geuza udongo mwekundu ni ishara mbaya inayoweza kuashiria ugonjwa unaoijia familia yako.

Kula Udongo

Kuota kuhusu kula udongo wa chokaa ama udongo mwekundu kunaweza kuashiria kwamba wewe ni mtu mwenye uhusiano na mizimu ama kwamba hivi punde utapata wito kutoka kwa mizimu.

Kuota kuhusu kula udongo kunaweza kuashiria jambo zuri. Kama unapitia hali fulani ngumu maishani mwako, basi ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba hali yako itakuwa bora zaidi. Lakini kama mambo yako yako vizuri tu nawe ukaota ndoto hii, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba utapitia changamoto na shida fulani maishani mwako.

Kama unaishi maisha mazuri nawe ukaota kwamba unakula udongo, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba utakutana na changamoto za kifedha.

Leave a Reply