Ndoto kuhusu mayai  

Kuna watu wanaoamini kwamba mayai katika ndoto huashiria uzao. Mtu akiota kwamba amekusanya mayai mengi bandani kwake, basi ndoto hiyo huonekana kuashiria kuwa mtu huyo atakuwa na uzao mkubwa. Hata hivyo, mtu anapoota kwamba mayai yamevunjika, basi ndoto hiyo hutafsiriwa kumaanisha kwamba uzao wa mtu huyo umeharibiwa ama kukamatwa na adui.

Wengine huamini kwamba, mayai katika ndoto huashiria mafanikio. Hivyo ukiota mayai mengi yako nyumbani mwako au kazini kwako, ndoto hiyo itaashiria kwamba utapata mafanikio kwenye ndoa yako, familia yako au kazini kwako. Lakini kama mayai hayo yameoza au yameharibika, basi ndoto hiyo itamaanisha kuwa uharibifu utaingia ama umekwishaingia kwenye mafanikio yako. 

Leave a Reply