Ndoto kuhusu kupigana

Kupigana katika ndoto kunaweza kuashiria mashambulizi anayopitia mtu iwe katika ndoa yake, uchumi wake, afya yake ama eneo lingine maishani mwake. Ukiota unapigana na mtu au mnyama kwenye ndoto nawe ukamshinda, basi ndoto hii huashiria kwamba kuna adui aliyekuwa akikufuatilia, lakini sasa umemshinda na hivyo hataweza kukuumiza tena.

Wakati mwingine kuota unapigana kunaweza kuashiria kwamba unapitia mapambano fulani katika harakati zako za kutafuta pesa, kazi, ndoa ama kitu kinginecho maishani. Mapambano haya yamaweza kuwa misukosuko ya kawaida apitiayo mtu maishani kama vile kukataliwa,  changamoto za pesa au mapenzi, n.k.

Wengine huamini kwamba mapigano katika ndoto huashiria vita ya kiroho. Vita hii inaweza kuhusisha maagano ya kale au laana zilizowekwa dhidi yako au dhidi ya kizazi ama familia yako.

Leave a Reply