Ndoto kuhusu kuku

Ukiota kuku wengi wanapiga kelele, basi ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba unapitia ushindani mkubwa kwenye eneo lako la kazi ama kwenye biashara yako. Ukiota kwamba kuku hao wanaingia nyumbani ama chumbani kwako, basi ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba ushindani huo umeingia kwenye familia ama kwenye ndoa yako, na wakati mwingine ndoto hii inaweza kuashiria uwepo wa matatizo fulani nyumbani kwako.

Mwanaume ambaye bado hajaoa akiota kwamba anachinja kuku, basi ndoto hiyo humaanisha kuwa mwanaume huyo ataoa msichana bikra siku za usoni. Kama atafanikiwa kumchinja pamoja na kumpika na kumla kuku huyo, basi ndoto hiyo itaashiria kwamba ndoa yake itakuwa ya amani, furaha na mafanikio. Lakini ikiwa kama kuku huyo atahangaika sana na kisha kumkimbia wakati alipokuwa akimchinja, jambo hilo litakuwa likimaanisha kwamba, ndoa yake haitafanikiwa na ikiwa atamwoa msichana huyo basi ndoa hiyo itavunjika.

Kuota kuku mweupe, mwenye rangi nzuri, mwenye afya, au mwenye manyonya mengi huashiria uwepo ama ujio wa mafanikio makubwa na ustawi katika maisha yako.

Msichana kuona jogoo katika ndoto humaanisha ujio wa mwenza au mume kwenye maisha yake. Vile vile aonapo vifaranga vingi kwenye ndoto, ndoto hiyo humaanisha kuwa msichana huyo atapata uzao mkubwa siku za mbeleni.

Leave a Reply