Kama ukiota kuhusu bunduki, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba kuna shida fulani inayokujia. Kama ukisikia mlio wa bunduki hiyo, basi unaweza kupatwa na ugonjwa ama mgogoro maishani mwako siku za hivi karibuni. Kama wewe ndiye unayefyatua bunduki hiyo, basi ndoto hii inaweza kuashiria jambo baya zaidi.
Ukiota umebeba bunduki ya uwindaji, ndoto hiyo humaanisha kwamba unapitia majira ya kutafuta jambo fulani kwenye maisha, iwe ni pesa, mke, mahala pa kuishi, matibabu au jambo jinginelo. Ndoto hii huashiria uwepo wa ujasiri na nia thabiti ya kukifuatilia kile unachokitaka.
Kuota watu waliobeba bunduki wakiwa wanakukimbiza ama kukufuatilia, humaanisha kwamba kuna vizuizi fulani vinavyozuia mafanikio na maendeleo yako.