Ndoto kuhusu sherehe ya harusiĀ 

Sherehe za harusi katika ndoto mara nyingi hutafsiriwa na watu kumaanisha ujio wa msiba. Kama una mgonjwa nyumbani mwako, na kisha mmoja wa wanafamilia yako akaota ndoto inayohusu sherehe ya harusi, basi kuna wanaoamini kwamba ndoto hiyo huashiria kwamba mgonjwa huyo atapoteza maisha.