Ndoto kuhusu Sinema
Kama ukiota kwamba unaenda kutizama sinema, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba utasafiri kwenda sehemu ya mbali.
Kama ukiota kwamba unaenda kutizama sinema, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba utasafiri kwenda sehemu ya mbali.
Kama ukiota kwamba upo gizani, hilo linaweza kuashiria ugumu fulani na umaskini siku zako zijazo, isipokuwa tu kama utaota kwamba umeweza kutembea kwenye giza hilo na kufikia sehemu yenye mwanga, kwani hilo litaashiria kuwa utastawi na kupata mafanikio.
Ndoto zinazohusu bidhaa za tumbaku zinaweza kubeba maana mbalimbali kulingana na aina na muktadha wa ndoto husika. Sigara Kuota kuhusu kuvuta sigara ni ishara mbaya inayoweza kukutahadharisha kuwa kuna hatari itakayokujia hivi punde maishani mwako kutokana na uzembe wako. Kuota kwamba unavuta sigara kunaweza kuashiria kwamba umelaaniwa, umerogwa, ama kwamba tatizo usilolifahamu ama usilolizingatia litaathiri …
Kama ukiota kuhusu mshumaa uliowashwa, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba huenda uko hatarini nawe unapaswa kuwa makini.
Kama ukiota kuhusu soko ama maduka, ndoto hiyo inaweza kuashiria bahati njema siku zako zijazo. Ndoto hii inaweza hata kuashiria jambo jema zaidi pale inapootwa na watu waliopo kwenye ndoa ama watu wanaouza vitu madukani.
Kama ukiota kuhusu hospitali, ndoto hiyo inaweza kuashiria jambo jema endapo kama ukiota kuwa unamtembelea mtu mwingine hospitalini hapo. Ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba utakuwa na afya nzuri. Lakini kama ukiota kwamba wewe ndiye umelazwa/unahudumiwa hospitalini hapo, ndoto hiyo itakuwa inakutahadharisha kuwa makini.
Kama ukiota kwamba unaishi ndani ya kibanda cha nyasi, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kuwa utagombana na rafiki yako siku si nyingi.
Kama ukiota kuhusu shamba, ndoto hiyo inaweza kuashiria mambo mazuri kwa ajili yako. Unaweza kupata mafanikio na furaha, hasa hasa endapo kama shamba hilo ni lako au kama ukiota kwamba unamsaidia mtu mwingine kuvuna matunda na mbogamboga shambani hapo.
Kama ukiota kuhusu mimea, maana ya ndoto hiyo itategemea namna mimea hiyo ilivyokua. Kama mimea hiyo imekua haraka, hilo linaweza kumaanisha kwamba mambo mazuri yatatokea, na yatatokea upesi. Kama mimea hiyo inakua polepole, basi hilo linaweza kumaanisha kwamba itakuchukua muda kiasi kupata mafanikio. Kama mimea hiyo inakua juu ya mwili wako, ndoto hii inaweza kuashiria …
Kama ukiona miguu yako au magoti yako kwenye ndoto, hilo linaweza kuashiria jambo zuri au baya. Kama miguu au magoti hayo ni dhaifu, unaweza kupatwa na bahati mbaya hasa hasa kama ukianguka kutokana na udhaifu wa miguu au magoti hayo. Lakini kama miguu au magoti hayo ni imara, basi unaweza kuwa imara na mwenye afya …