Kama ukiona miguu yako au magoti yako kwenye ndoto, hilo linaweza kuashiria jambo zuri au baya. Kama miguu au magoti hayo ni dhaifu, unaweza kupatwa na bahati mbaya hasa hasa kama ukianguka kutokana na udhaifu wa miguu au magoti hayo. Lakini kama miguu au magoti hayo ni imara, basi unaweza kuwa imara na mwenye afya maishani mwako, hasa hasa kama wewe ni mwanaume. Kwa upande mwingine, kama wewe ni mwanamke, ndoto hiyo kwa kawaida humaanisha kuwa mume wako atakutunza na kuwa mwema kwako.