Ndoto kuhusu Jongoo

Mahusiano na Mababu Kama majina ya watu wa ukoo wako yanajumuisha majina kama ‘Bhengu’, basi ndoto ihusuyo jongoo inaweza kuwa ishara kutoka kwa mababu zako. Tahadhari na Vitisho Kuota kuhusu kukutana na jongoo wakati ukiwa unatembea nje kunaweza kuashiria kwamba unapaswa kuwa makini kwani kuna mtu asiyekutakia mema, anayetaka kukusaliti ama kukuroga. Kuota kwamba unamuona …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Funza

Kuota kuhusu funza kunaweza kuashiria ugonjwa, uchawi, ama watu wabaya waliopo maishani mwako. Funza Mwilini Mwako Kuota kwamba una funza mwilini mwako kunaweza kumaanisha kuwa unarogwa. Wakati mwingine, kuota kuhusu funza kunaweza kumaanisha kwamba unahofu kuhusu matatizo unayohitaji kuyatatua. Ndoto hii inaweza pia kumaanisha kuwa kuna hasira ya Mungu unayokumbana nayo kutokana na vitendo vyako …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Chawa

Kama ukiota kuhusu chawa, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba utakutana na shida fulani maishani mwako, hasa hasa kazini kwako. Hakikisha unalipa madeni yako na unachunga afya yako.

Ndoto kuhusu Nzi

Kama ukiota kuhusu nzi, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna watu wanaokuonea wivu, wanaoweza kujaribu kukuingiza matatizoni.

Ndoto kuhusu Shimo

Kama ukiota kuhusu shimo lililopo ardhini, ndoto hii inaweza kuashiria jambo zuri ikiwa kama shimo hilo ni tupu, kwani hilo linaweza kuashiria kuwa utapata familia yenye hisia za furaha na kuheshimiana. Lakini kama ukiota kwamba shimo hilo limejaa maji, basi ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba kuna mambo mabaya yanayokujia.

Ndoto kuhusu Mteremko Mkali wa Mwamba/Mlima

Kama ukiota kuhusu mteremko mkali wa mwamba/mlima, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba kuna jambo muhimu litatokea kwenye mahusiano yako siku za hivi karibuni. Ndoto hii inaweza kuashiria uwepo wa mtoto siku zako za usoni. Lakini, kama ukiota kwamba unaning’inia kwenye mteremko mkali wa mwamba/mlima na kuna mtu amekushika mkono usianguke, basi hilo linaweza kumaanisha kwamba …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Kichaka

Kama ukiota kwamba unatembea kwenye kichaka, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba kutatokea mabadiliko fulani kwenye maisha yako, nawe unaweza kuhama nyumba ama kubadili ajira yako hivi karibuni.

Ndoto kuhusu Mzeituni Mwitu

Kama ukiota kuhusu mzeituni mwitu, na ukaona tunda kwenye matawi ya mzeituni huo, basi ndoto hii inaweza kuashiria maisha ya amani na furaha, utakayoweza kutimiza matamanio yako yote.

Ndoto kuhusu Mbao/Kuni

Ndoto zihusuzo mbao/kuni zinaweza kuwa na maana nzuri na mbaya kulingana na muktadha husika. Kukusanya na Kubeba Mbao/Kuni Kama ukiota kwamba unatafuta mbao/kuni ama unajaribu kukusanya kuni lakini haupati zozote,hii inaweza kuwa ishara nzuri inayoashiria kwamba hautashirikiana na watu wabaya wasambazao maneno mabaya na kusababisha matatizo kwenye maisha ya watu wengine. Hata hivyo, wakati mwingine …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Miiba

Kwa kawaida, kuota kuhusu miiba kunaweza kuashiria tatizo, jambo baya, ama hali ya kushindwa. Hata hivyo, maana halisi hutegemeana na hali husika na kile kilichotokea kwenye ndoto. Miiba Mwilini Mwako Tafsiri ya ndoto inayohusu kuwa na miiba mikononi mwako kwa kawaida huhusiana na kazi yako. Huenda kuna watu kazini kwako wasiopenda namna unavyofanya vitu, ama …

Soma zaidi