Kuota kuhusu funza kunaweza kuashiria ugonjwa, uchawi, ama watu wabaya waliopo maishani mwako.
Funza Mwilini Mwako
Kuota kwamba una funza mwilini mwako kunaweza kumaanisha kuwa unarogwa. Wakati mwingine, kuota kuhusu funza kunaweza kumaanisha kwamba unahofu kuhusu matatizo unayohitaji kuyatatua. Ndoto hii inaweza pia kumaanisha kuwa kuna hasira ya Mungu unayokumbana nayo kutokana na vitendo vyako viovu. Kuota kuhusu funza wakitembea mwilini mwako kunaweza kuashiria kwamba umezungukwa na watu wabaya wanaoweza kukuumiza ikiwa kama watapata nafasi ya kufanya hivyo.
Mwili wako Kutokwa na Funza
Kama unaumwa, nawe ukaota kwamba mwili wako unatokwa na funza, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba utapona. Kama ukiota kwamba funza wanatoka mwilini mwako, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa mauti inatoka mwilini mwako na hivyo utakuwa na afya zaidi. Wakati mwingine, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa unaondokana na matatizo, nguvu za giza, ama uchawi.
Kuota kuhusu kutokwa na funza kunaweza kuashiria kujitenga kwa watu wabaya waliokuwa karibu na wewe. Kama ukiota kwamba mpenzi/mwenzi wako anatokwa na funza kwenye sehemu zake za siri, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba mtu huyo alifanya mapenzi na mtu mbaya aliyemrushia uchawi unaoweza kuwa unakuathiri wewe pia.