Ndoto kuhusu Mbao/Kuni

Ndoto zihusuzo mbao/kuni zinaweza kuwa na maana nzuri na mbaya kulingana na muktadha husika.

Kukusanya na Kubeba Mbao/Kuni

Kama ukiota kwamba unatafuta mbao/kuni ama unajaribu kukusanya kuni lakini haupati zozote,hii inaweza kuwa ishara nzuri inayoashiria kwamba hautashirikiana na watu wabaya wasambazao maneno mabaya na kusababisha matatizo kwenye maisha ya watu wengine. Hata hivyo, wakati mwingine kuota kuhusu kushindwa kupata kuni/mbao kunaweza kuashiria jambo baya, kunaweza kuashiria umaskini, ufukara na kushindwa kupata msaada.

Kuota kuhusu kukusanya kuni ama kuota kuhusu mzigo wa kuni kunaweza kunaweza kuashiria jambo hasi na kwamba unapaswa kusubiri na kusali kwani huzuni na maradhi yanaweza kukujia hivi karibuni.

Kama ukiota kwamba umebeba kifurushi cha kuni, hii ni ishara mbaya inayoweza kuashiria fedheha, kuadhibishwa, kutendewa kwa ukatili, na kunyanyaswa na watu wabaya na wachawi wasiokutakia mema.

Kama ukiota kwamba unamkusanyia mtu mwingine kuni, hii ni ishara njema inayoashiria kwamba wewe ni mtu mwenye heshima, unayejali watu, mwema, mwenye upendo, na kwamba wewe ni baraka kwa watu wengine.

Kupokea na Kununua Mbao/Kuni

Kama ukiota kwamba unapatiwa mbao/kuni na mtu mwingine, hii ni ishara njema inayoweza kuashiria baraka, kuheshimiwa, na kwamba Mungu atakutimizia mahitaji yako.

Kama ukiota kwamba unanunua kuni/mbao, hii inaweza kuwa ishara mbaya inayoashiria mateso, taabu na umaskini unaoweza kukumbana nao utakaosababishiwa na watu wasio na utu wala huruma.

Leave a Reply