Ukiota unaandika barua ama taarifa fulani, basi ndoto hiyo huashiria kwamba kuna ujumbe unaopaswa kupata kutoka kwa mababu zako ama kutoka kwa muumba wako, nawe hauna budi kuutendea kazi ama kuufikisha ujumbe huo kwa mtu au eneo husika.
Kama ukiota kwamba unachora ramani ya eneo fulani, basi ndoto hiyo humaanisha kwamba unatakiwa kufikiri kwa kina zaidi kuhusiana na uamuzi fulani utakaochukua, ama kuchunguza kwa ukaribu zaidi suala fulani maishani mwako.
Ukiota unapaka rangi kwenye ukuta, ndoto hii huashiria mwanzo mpya.
Kama mama mjamzito akiota anajichora ama amechorwa michoro mizuri ya henna mwilini mwake, ndoto hii huashiria hisia za furaha, uangavu na uzuri wa mwanamke huyo. Lakini kama michoro hiyo itaonekana kuwa haieleweki na iliyovurugwa-vurugwa, basi ndoto hiyo itakuwa inaashiria mvurugiko wa kihisia, wasiwasi au hofu aliyonayo mwanamke huyo kuhusiana na ujauzito husika.
Mwanamke ambaye bado hajaolewa, akiota kwamba amechorwa henna mwilini mwake, basi ndoto hii huashiria ujio wa sherehe au harusi maishani mwa mwanamke huyo. Ndoto hiyo huashiria kuwa siku za hivi karibuni, mwanamke huyo atapata furaha, utulivu au baraka fulani maishani mwake.