Kuota kuhusu ndege kunaweza kuashiria mambo mengi. Kuota kwamba unawasikia ndege wakiimba kunaweza kuashiria kwamba kuna shida inayokujia. Kuota kwamba unaona ndege wakipaa hewani kunaweza kuashiria kwamba utasalitiwa na watu uliodhani kwamba unaweza kuwaamini. Kuota kwamba unawaona ndege wakiwa mwituni kunaweza kuashiria kuwa utapokea habari usizozitarajia. Kuota kuhusu kundi kubwa la ndege kunaweza kuashiria mafanikio kama wewe ni mtu tajiri. Wakati kuota kuhusu kundi dogo la ndege kunaweza kuashiria mafanikio kama wewe ni mtu maskini.