Ndoto kuhusu Moto  

Kama ukiota kuhusu moto ama miale ya moto, ndoto huu huaminika kuashiria jambo baya litakalotokea siku zako zijazo. Ndoto hii inaweza kuashiria kwamba huko mbeleni utapatwa na hisia za hasia na usaliti. Unaweza ukapoteza vitu muhimu kwako na hata kukumbana na ugonjwa na mauti. Kama ukiota kwamba unauchochea moto huo kuwaka zaidi, basi hilo linaweza kuashiria kuwa utagombana na mtu unayemfahamu.

Ndoto zinazohusu moto zinaweza kutofautiana maana kutegemeana na muktadha wa ndoto husika. Kwa mfano:

  • Ukiota vitu vyako vinateketea kwa moto, basi ndoto hiyo humaanisha kwamba unaenda kuingia hasara ama kufilisika na kupoteza utajiri wako.
  • Ukiota unapita katika moto na kisha kutokea upande mwingine, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba unapitia ama utapitia jambo gumu la kukuimarisha, lakini mwishowe utapata ushindi.
  • Ukiota kwamba uko ndani ya moto lakini hauungui wala kuteketea, ndoto hii inaweza kuashiria kusafishwa ama kutakaswa kwa matendo yako mabaya.
  • Ukiota kwamba moto ulikuwa unawaka na kisha ukazimika ghafla, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba kuna jambo baya litakalokujia ghafla na kusababisha giza ama matatizo kwenye maisha yako.
  • Ukiota kwamba upo katikati na umezungukwa na miale ya moto, basi ndoto hii inaweza kuashiria kwamba umezungukwa na roho za mababu zako zinazokulinda usipatwe na mabaya.
  • Ndoto za moto zinaweza pia kuashiria shughuli za kichawi ama vitendo vya kishirikina. Kwa mfano unapoota mti au gogo linateketea kwa moto, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba kuna mtu anafanya uchawi dhidi yako au familia yako ili kuwateketeza.

Leave a Reply