Ndoto zinazohusu miwa kwa kawaida huashiria mambo mazuri.
Kula Muwa
Kuota kuhusu kula muwa ni ishara njema, inaweza kuashiria kwamba nyakati nzuri zitakujia, utapata furaha na bahati maishani, na kwamba utapata maendeleo. Kuota kuhusu kula muwa kunaweza kuashiria kupata upendo, wema, heshima na matunzo kutoka kwa watu wako wa karibu.
Mashamba ya Miwa
Kuota kwamba unaotesha miwa, unavuna miwa ama kuhusu shamba la miwa ni ishara njema. Inaweza kuashiria kwamba utapata bahati na mafanikio kwenye kile unachokifanya. Inaweza pia kuashiria kwamba utapata furaha, masumbuko yako yataisha, utapiga hatua, utapata utajiri ama utanufaika kutokana na jitihada zote ulizoziwekeza kwenye maisha yako.
Kuvuna Miwa
Kuota kwamba unavuna miwa kunaweza kuashiria kwamba utapitia changamoto fulani kabla ya kuzitimiza ndoto zako. Wakati mwingine, ndoto hii humaanisha kwamba unapaswa kubadili hisia na fikra zako, na kutathmini ni mambo gani unayopaswa kuyazingatia na yapi unayopaswa kupuuzia, hasa hasa endapo kama umepitia nyakati ngumu.
Kuota kuhusu shamba linalolimwa kwa plau, jembe ama linalooteshwa mazao ni ishara mbaya inayoweza kumaanisha kwamba mtu wa familia yako ama ndugu yako atapatwa na ugonjwa siku za hivi karibuni.
Kununua Miwa
Kuota kuhusu kununua miwa kunaweza kuashiria hatua mpya maishani, kwamba una matumaini na unaamini katika kile unachokifanya. Hata hivyo, maana ya ndoto hii hutegemeana na hisia za mtu aliyeiota. Wakati mwingine, ndoto hii inaweza kuashiria hisia za upweke, mahangaiko, hofu ya kushindwa jambo, na hisia za kukosa muelekeo maishani.