Ndoto kuhusu kuoga 

Ukiota kwamba unaoga, ndoto hii inaweza kumaanisha mambo mazuri au mambo mabaya. Kama maji unayoogea yametulia ama kama unaoga ukiwa bafuni kwako, ndoto hii humaanisha kwamba utapata bahati njema hivi karibuni ama utahamia eneo lingine na kupata furaha. Lakini kama ukiota unaoga nje ama unaoga kwenye maji yanayotiririka, ndoto hii huonekana kumaanisha kwamba utapatwa na jambo baya ama kukatishwa tamaa. 

Kuna wanaoamini kwamba, kama ukiota unaoga kwenye bafu chafu, basi ndoto hiyo humaanisha kwamba mababu zako ama muumba wako anakukumbusha kuwa matendo yako ni mabaya na unapaswa kujitakasa. 

Ukiota unaoga hadharani ama mbele za watu, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna jambo la aibu linaloenda kukupata kazini kwako, nyumbani kwako, mtaani kwako, kwenye biashara yako ama eneo lengine maishani mwako siku zijazo.

Leave a Reply