Ndoto kuhusu Mzeituni Mwitu
Kama ukiota kuhusu mzeituni mwitu, na ukaona tunda kwenye matawi ya mzeituni huo, basi ndoto hii inaweza kuashiria maisha ya amani na furaha, utakayoweza kutimiza matamanio yako yote.
Kama ukiota kuhusu mzeituni mwitu, na ukaona tunda kwenye matawi ya mzeituni huo, basi ndoto hii inaweza kuashiria maisha ya amani na furaha, utakayoweza kutimiza matamanio yako yote.
Kama ukiota kwamba unatembea kwenye kichaka, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba kutatokea mabadiliko fulani kwenye maisha yako, nawe unaweza kuhama nyumba ama kubadili ajira yako hivi karibuni.
Kama ukiota kuhusu jangwa, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba unaweza ukakutana na jambo baya katika siku zako zijazo.
Kama ukiota kuhusu mvua ya mawe, ndoto hii inaweza kuashiria mambo mabaya yajayo. Unaweza ukapoteza ajira yako ama kuwapoteza watu unaowajali, kama hautakuwa makini. Pia, siri unazozificha zinaweza zikafichuliwa.
Kama ukiota kwamba unapatiwa ubani, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba unapatiwa mamlaka ya kuiongoza kaya yako na kuzungumza na mababu zako. Kwa kawaida hili hutokea pindi panapokuwa hakuna mzee yoyote tena kwenye familia ama kwa mtoto ‘aliyezaliwa kwa ajili ya wajomba’. Basi hali hii hukutaka kutafuta kaya yenye mahusiano ya moja kwa moja na wewe, …
Kama ukiota kuhusu tetemeko la ardhi, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba utapoteza vitu vyako muhimu.
Kama ukiota kuhusu barafu, maana ya ndoto hiyo itategemea wewe ni nani. Kwa wakulima, ndoto hii inaweza kuashiria bahati mbaya na mavuno machache, lakini kwa wapendanao, ndoto hii inaweza kuashiria ndoa na furaha.
Kama ukiota kuhusu majani ya mti, ndoto hii inaweza kuashiria mambo mazuri ikiwa kama majani hayo ni ya kijani na bado yameambatana na mti husika. Ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba utafanikiwa na kustawi katika mambo yale unayoyafanya. Lakini kama ukiota kuhusu majani yaliyoanguka ardhini kutoka kwenye mti, basi unaweza kupitia mateso kutokana na vitendo vya …
Kama ukiota kuhusu kilima chenye mwinuko mkali ulio mgumu kupanda, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba utapitia taabu fulani lakini mwishowe utafanikiwa maishani mwako.
Kama ukiota kuhusu uyoga, ndoto hiyo inaweza kuashiria jambo jema ikiwa kama ukiota kuwa unavuna uyoga huo. Lakini huashiria jambo baya kama ukiota kwamba unakula uyoga huo – hasa hasa kama ukiota kwamba umeumwa baada ya kula uyoga huo.