Ndoto kuhusu Kusikia Muziki

Kama ukiota kwamba unasikia muziki wa furaha, hili humaanisha kuwa utapata habari njema hivi karibuni. Lakini kama ukisikia muziki wa huzuni kwenye ndoto yako, hili humaanisha kwamba utapata habari mbaya.

Ndoto kuhusu Kusikia Redio

Kama ukiota kwamba unasikia redio, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa unapaswa kumpigia simu ama kumtembelea ndugu yako ambaye hujaonana nae hivi karibuni.

Ndoto kuhusu Shindano la Mbio

Kama ukiota kwamba unashiriki kwenye shindano la mbio, hii ni ishara njema, ilmradi tu usianguke kwenye mbio hizo. Kama utaibuka mshindi, basi utapata mafanikio hivi karibuni, lakini kama ukipoteza ushindi, hali hiyo inaweza kuashiria jambo baya.

Ndoto kuhusu Kuogelea

Kama ukiota kwamba unaogelea, ni ishara njema ikiwa kama kichwa chako kitakuwa juu ya maji. Maana ya ndoto hii huhusiana hasa hasa na masuala ya kazi na mahusiano. Kama maji hayo ni masafi na meupe, basi ndoto hiyo ni nzuri. Kama unaogelea huku kichwa chako kikiwa ndani ya maji, hili humaanisha kuwa kuna shida inayokujia, …

Soma zaidi