Ndoto kuhusu Washawasha (Mdudu Mopane)

Kama ukiota kuhusu wadudu washawasha hii ni ishara mbaya inayoashiria kuwa umewaruhusu watu wabaya wajenge ukaribu na wewe, na kwamba unaweza kushambuliwa na roho chafu ulizorushiwa. Unapaswa kutafuta uponyaji. Kama ukiota kuhusu mdudu huyu, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba unapaswa kuwa makini kwani kuna watu wanaopanga njama dhidi yako. Kama ukiota kuwa kuna washawasha wengi …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Chura

Kama ukiota kuhusu chura, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba utafanikiwa na kupata utajiri.

Ndoto kuhusu Mjusi

Kama ukiota kuhusu mjusi, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba kuna mtu wa familia yako atakusaliti.

Ndoto kuhusu Kichuguu

Kuota kwamba unatizama kichuguu kilichopo uwani nyumbani ni ishara mbaya inayoweza kuashiria kaburi au kuashiria kwamba kuna mtu atafariki na hakuna chochote unachoweza kukifanya ili kumuokoa mtu huyo. Kama ukiota kuhusu kichuguu, ndoto hii inaweza kuwa ishara inayoashiria kwamba unapaswa kujitahadhari na jambo baya litakalokupata hivi karibuni. Kuota kuhusu kichuguu kunaweza kumaanisha kwamba utakuwa mpweke …

Soma zaidi

Ndoto kuhusu Mnyoo

Kama ukiota kuhusu minyoo, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna watu wanaotaka kukusababishia madhara.

Ndoto kuhusu Buibui

Kama ukiota kuhusu buibui, ama utando wa buibui, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa kuna mambo mazuri yanayokujia. Pengine utapata fedha pasipo kutarajia, ama kuna mtu atakutembelea hivi karibuni.

Ndoto kuhusu Kumbikumbi

Kama ukiota kuhusu kumbikumbi, ndoto hii inaweza kumaanisha kuwa kuna hatari unayosababishiwa na watu uliodhani kuwa unaweza kuwaamini.

Ndoto kuhusu Nyigu

Kama ukiota kuhusu nyigu, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba una maadui wanaokutakia madhara. Kama ukiota kwamba mmoja wa nyigu hao amekuuma, basi ndoto hii inaweza kuashiria kuwa utaingia matatizoni. Lakini kama ukiota kwamba umemuuwa mmoja wa nyugi hao, hilo linaweza kuashiria kwamba utafanikiwa.