Ndoto kuhusu Chura
Kama ukiota kuhusu chura, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba utafanikiwa na kupata utajiri.
Kama ukiota kuhusu chura, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba utafanikiwa na kupata utajiri.
Kama ukiota kuhusu wadudu washawasha hii ni ishara mbaya inayoashiria kuwa umewaruhusu watu wabaya wajenge ukaribu na wewe, na kwamba unaweza kushambuliwa na roho chafu ulizorushiwa. Unapaswa kutafuta uponyaji. Kama ukiota kuhusu mdudu huyu, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba unapaswa kuwa makini kwani kuna watu wanaopanga njama dhidi yako. Kama ukiota kuwa kuna washawasha wengi …
Kama ukiota kuhusu minyoo, ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba kuna watu wanaotaka kukusababishia madhara.
Ndoto zinazohusu kiota cha ndege zinaweza kuashiria jambo jema, almradi tu kiota hicho kiwe na mayai ndani yake. Hata hivyo, kama kiota hicho ni kitupu, ndoto hiyo inaweza kuashiria kwamba unahitaji kujitahadhari na shida fulani.
Kuota kuhusu msingwe kunaweza kuashiria jambo baya kwako, hasa hasa kama ukiota kwamba umemuuwa msingwe huyo.
Kuota kuhusu kundi la ndege kunaweza kuashiria ujio wa bahati njema na ustawi siku zako zijazo. Kama ukiota kwamba unawafuga ndege hao, ndoto hii inaweza kuashiria kuwa biashara yako itafanikiwa sana hivi karibuni, na utanufaika sana kutokana na biashara hiyo.
Kama ukiota kuhusu majani/nyasi, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba utapata furaha na mafanikio siku zako zijazo, hasa hasa kama majani/nyasi hizo zikiwa za kijani na zilizostawi. Hata hivyo kama ukiota kuhusu majani/nyasi zilizokufa, ama ukiota kwamba unakata majani/nyasi, ndoto hiyo itaashiria kwamba utakuwa na bahati mbaya na huzuni.
Kama ukiota kwamba kuna msitu mdogo karibu na nyumba yako, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba ndoa yako itakuwa na furaha, nanyi mtapata watoto wengi.
Kama ukiota kuhusu mmea wa mziwaziwa, ndoto hiyo inaweza kumaanisha kwamba utakuwa na bahati njema, hasa kwenye mahusiano yako. Kama bado haujaoa/haujaolewa, au haupo kwenye mahusiano ya kimapenzi, basi ndoto hii inaweza kumaanisha kwamba utapata mwenzi ama utaoa/utaolewa siku za hivi karibuni.
Kama ukiota kuhusu mmea wa bangi, ndoto hii inaweza kuashiria kwamba unahitaji kuchukua muda kutafakari kuhusiana na maisha yako badala ya kukurupukia tu mambo.